Wednesday, January 13, 2010

DUKE GET BUSY WITH THT AND MALARIA PROJECT

Ni kama mwaka umeanza vizuri kwa upande mmoja na mbaya kwa upande wa pili kwa Producer DUKE. Umeanza vibaya kwa kuwa amelazimika kuikatisha likizo yake kutokana na ratiba ndeefu ya project zinazomkabili.

Kwa upande wa habari nzuri ni kuwa, Baada ya kulisuka vilivyo lile project la gospel la mwanadada Jessica Honore linalojulikana kwa jina la "TENZI ZA ROHONI", The super dupa producer amekuwa busy sana na project ya THT ikiwahusisha AMIN na nyimbo yake inayosumbua sana redioni ikifahamika kama "Robo saa" mbali na mwanamuziki huyo, tayari kashamaliza mzigo wa wanadada Lina, Jane na Jasmeen ikiwa nyimbo zote hizi ndizo zilizofungulia mwaka katika station mbalimbali za radio. Mbali na tracks hizo kuna nyimbo ya barnaba na Lina ambayo inafanyiwa mixing kabla ya kudondoshwa kwa radio.

Hivi sasa amekuwa busy sana na nyimbo ya kuhamasisha vita ya kutokomeza malaria ambayo mratibu mkuu wa project ya wimbo huo ni ndugu Ruge mutahaba. Nyimbo hiyo imesheheni mastaa kibao wa kzazi kipya na baadhi wa zamani kama Bi. Kidude, pia yupoLady Jay Dee, Marlaw, Barnaba, Amini, Grace matata, Lina,Mwasiti, Proffesor J,Banana,Madii,Keisha,Mataaruma,Jane, na wengineo wakitimiza idadi ya mastaa 18 ambao watakuwa katika track hiyo itakayoanza kurushwa hewani mwishoni mwa wiki hii huku ikizinduliwa na waziri wa afya Proff. mwakyusa hapo tarehe 14/january/2010

wakati huo huo, ili kudhihirishia watu kuwa mwaka huu kapania kufunia kabisa, ule mwimbo wa mchiriku ulio katika project moja ya clouds ikiwa ni production yake mzee mzima..umeshaingia redioni kwa vurugu nyingi sana.Aidha, mratibu wa project hiyo, bwana Athuman shaaban maarufu kwa jina la SUKA hakupatikana kutolea ufafanuzi wa project hiyo nzima ya mchiriku.

mLAB inamtakia kazi njema mzee mzima duke na team yake nzima ya ufinyanzi na uhunzi wa milio ili wote wale wabishi wakae chini pasi kutambaa

1 comment:

Anonymous said...

Hi, after reading this awesome piece of writing i am as well delighted to share my
know-how here with mates.

my website: www.fdw.fr